Mpox, ugonjwa hatari wa kuambukiza ambao huambukizwa na Nyani umetangazwa kuwa ugonjwa wa hatari barani Afrika na bodi kuu ya afya ya bara hilo.
Wanasayansi kutoka Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) wanasema wanasikitishwa na kasi ambayo aina hiyo mpya ya ugonjwa huo umekuwa ukienea.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, zaidi ya maambukizi 13,700 na vifo 450 vimerekodiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Virusi hivyo vinavyoweza kusababisha vidonda katika mwili mzima vimesambaa hadi katika mataifa mengine ya Afrika, zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Kenya na Rwanda.

