Kundi la Hamas limesema haitajiunga na mazungumzo ya kusitisha mapigano wiki hii.
Mazungumzo yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi kujadili usitishaji vita kati ya Israel na Hamas.
Hata hivyo, mwakilishi wa Hamas nchini Lebanon aliiambia Sky News kwamba wajumbe kutoka kundi la wanamgambo hawatashiriki tena mazungumzo hayo.
Katika taarifa yake, Ahmad Abdul Hadi alisema Hamas haipingani na mazungumzo ya kusitisha mapigano “kimsingi”.
Hata hivyo, alisema haitashiriki wiki hii kwa sababu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu “hataki kufikia makubaliano ambayo yatamaliza uchokozi wa Israel “.

