Jeshi Polisi mkoa wa Dodoma, linamshikilia mlinzi wa Kanisa Raphael mwenye miaka 26 Keneth Ndamahnwa kuhusiana na kifo cha msanii Mandojo aliyefariki kutokana na kipigo akidhaniwa kuwa ni mwizi.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, kijana huyo ni mlinzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Watakatifu Wote, lililopo Nzuguni B.
Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo inasema anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kifo cha Mandojo, ambaye jina lake halisi ni Joseph Francis kilochotokea Agosti 11 mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi SACP. Anania Amo amesema kuwa Jeshi hilo, linaendelea kumuhoji Raphael Keneth, kuhusiana na tukio hilo.
Kamanda Anania amesema mwili huo umefanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo chake.
Iliripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa Mandojo alipigwa kwa kudhaniwa ni mwizi.

