KMC yamkaribisha Awesu baada ya kushinda kesi dhidi ya Simba

KMC yamkaribisha Awesu baada ya kushinda kesi dhidi ya Simba

Timu ya KMC imemkaribisha klabuni hapo Awesu Awesu baada ya kushinda kesi dhidi ya Simba kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini ( TFF).

Kwa hatua hiyo, Awesu ni mali ya KMC sio Simba baada ya kushinda shauri hilo.

A, mchezaji huyo alitangazwa kama mchezaji mpya wa Simba Sc kuelekea msimu mpya wa 2024/25 jambo lililozua sintofahamu huku Wakusanya Ushuru hao wa Jiji la Dar es Salaam wakidai Simba Sc wamemsajili nyota huyo wa zamani wa Madini FC bila kufuata taratibu.

Mwanasheria wa Klabu ya KMC , Cheaf Said alisema Awesu bado ni mali ya klabu hiyo na kama Simba wakimtaka warudi mezani kwa ajili ya mazungumzo wakiwa na Tsh milioni 200.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *