Mama, watoto wake mapacha wauawa shambulio la Israel

Mama, watoto wake mapacha wauawa shambulio la Israel

Mama pamoja na watoto wake wachanga mapacha wenye umri wa siku nne tu wameuawa katika shambulio la anga la Israel huko Gaza.

Shambulio hilo lilitokea wakati baba wa watoto hao alipokwenda katika ofisi ya serikali ya mtaa kuandikisha kuzaliwa kwao.

Watoto hao, Asser ambaye ni mvulana na Ayssel ambaye ni msichana, walikuwa na umri wa siku nne tu wakati baba yao Mohammed Abu al-Qumsan alipokwenda kuchukua vyeti vyao vya kuzaliwa.

Akiwa mbali, majirani zake wamlipiga simu baba yao na kumwambia kuwa nyumba yao huko Deir al Balah ilikuwa imelipuliwa.

Shambulio hilo pia liliua mkewe na nyanya wa mapacha hao.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *