Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema kuwa hataomba kuchaguliwa tena kama kiongozi wa chama tawala cha Liberal Democratic Party (LDP), ambacho anasema kinahitaji “mwanzo mpya”.
Mwanasiasa huyo mkongwe huyo wa LDP mwenye umri wa miaka 67 anatarajiwa kujiuzulu kama Waziri Mkuu baada ya chama kumchagua kiongozi mpya mwezi Septemba.
Uungwaji mkono wa Bw Kishida, ambaye amekuwa Waziri Mkuu tangu 2021, umeangukia katika kashfa ya ufisadi iliyohusisha chama chake, kupanda kwa gharama za maisha na pesa ya nchi hiyo (Yen) kushuka.

