TANESCO MARA YAJIVUNIA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

TANESCO MARA YAJIVUNIA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Watumishi katika Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoani Mara, wamesema uboreshaji na uimara wa huduma wanazozitoa kwa Wananchi ni kutokana na Serikali kuongeza vitendea kazi ikiwemo Magari matatu pamoja na Babaji zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wananchi katika mkoa huo.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara Mhandisi Ezekia Mashola wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi ambapo katika mkoa wa Mara yamefanyika Wilayani Bunda ambapo amesema kama Shirika hawana budi kuishukuru Serikali kwa kufanikisha, kuboresha na kutoa huduma kwa Wananchi.

Mhandisi Mashola amesema pamoja na mafanikio hayo lakini pia kuna mafanikio makubwa hususani kwa Wafanyakazi waliokuwa na mikataba ya muda sasa wamepewa mikataba ambayo itawafanya kufanya kazi kwa furaha hivyo maadhimisho hayo ni faraja kwa Shirika hilo kutokana nnamna serikali inavyosikiliza na kutatua nchangamoto za Wafanyakazi wake.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *