Britney Spears ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Britney Spears ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Mwimbaji maarufu wa Pop, Britney Spears, mwenye umri wa miaka 44, ameshtakiwa rasmi kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa pombe na dawa za kulevya (DUI), kufuatia tukio la kukamatwa kwake mwezi Machi mwaka 2026 huko Kaunti ya Ventura, California.

Kwa mujibu wa Mamlaka, Spears alikamatwa tarehe 4 Machi baada ya Polisi kumuona akiendesha gari lake aina ya BMW kwa mwendo usio wa kawaida, akibadilisha njia barabarani na kuonyesha dalili za kulewa. Baada ya kusimamishwa, alifanyiwa vipimo vya ulevi ambavyo alishindwa, jambo lililopelekea kukamatwa kwake mara moja.

Baada ya tukio hilo, alipelekwa kituo cha Polisi na kushikiliwa kwa muda kabla ya kuachiwa kwa dhamana siku iliyofuata. Hakuna ajali au majeruhi yaliyoripotiwa kutokana na tukio hilo.

Waendesha mashtaka wamemfungulia shtaka moja la kosa la kiwango cha chini (misdemeanor), na wanaweza kumpa makubaliano ya kukiri kosa la “uendeshaji hatarishi unaohusisha pombe au dawa” (wet reckless). Endapo atakubali, huenda akaepuka kifungo jela na badala yake apewe adhabu kama:

  • miezi 12 ya uangalizi (probation),
  • kuhudhuria programu ya elimu ya ulevi,
  • pamoja na kulipa faini.

Inaripotiwa pia kuwa baada ya tukio hilo, Spears alijitolea kujiunga na kituo cha matibabu ya uraibu mwezi Aprili ili kushughulikia hali yake na kuimarisha afya yake ya akili.

Kesi yake inatarajiwa kusikilizwa mahakamani tarehe 4 Mei, ingawa si lazima yeye binafsi kuhudhuria kwa kuwa shtaka hilo ni la kiwango cha chini.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *