Liverpool yamkosesha usingizi Mikel Arteta

Liverpool yamkosesha usingizi Mikel Arteta

Mikel Arteta amewataka wachezaji wake kupambana ili kuibania Liverpool ubingwa wa taji la Premier League.

Vijana wa Arteta wanaingia kwenye mpambano wao wa Siku ya Mwaka Mpya na Brentford wakiwa nyuma kwa alama tisa nyuma ya vinara wa msimamo Liverpool.

Wachezaji hao wa Anfield wameshinda mechi 14 kati ya 18 za ligi msimu huu na kuwafanya wapewe nafasi nzuri ya kutwaa taji ambalo Arsenal wanalitarajia pia msimu huu.

Huku mabingwa Manchester City wakiwa na msukosuko, washika nafasi ya tatu wa Gunners walitarajia kufaidika baada ya kumaliza kama washindi wa pili kwa miaka miwili iliyopita.

Lakini Arsenal hali hiyo imemchosha Arteta na kutoa kilio chake kabla ya mechi yao ya mwisho ya 2024.

“Lazima tuendelee kuwa wagumu ili tushinde,” amesema.

Arsenal wanawania kushinda taji lao la kwanza tangu 2004, lakini watakuwa bila Bukayo Saka kwa kipindi kirefu baada ya winga huyo wa Uingereza kukaa nje hadi angalau mwezu Machi kutokana na jeraha la misuli ya paja.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *