Amorin: Tunapambana tusishuke daraja

Amorin: Tunapambana tusishuke daraja

Ruben Amorim amesema kuwa Manchester United iko kwenye vita ya kunusurika kwenye Ligi ya Premia baada ya kufungwa 2-0 na Newcastle Jumatatu na kumaliza 2024 katika nafasi ya 14 kwenye jedwali.

United wako pointi saba juu ya eneo la kushushwa daraja, lakini wako kwenye mteremko tangu Amorim achukue usukani mwezi uliopita.

Alexander Isak na Joelinton walifunga ndani ya dakika 19 za kwanza United ikipoteza mchezo wa tatu mfululizo wa ligi ya nyumbani tangu 1979.

“Hilo liko wazi kwa hivyo lazima tupambane,” alisema Amorim kuhusu United kuburuzwa kwenye vita vya kushuka daraja.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *