Ripoti: Ndege iliyoanguka ilikuwa haina shida yoyote

Ripoti: Ndege iliyoanguka ilikuwa haina shida yoyote

Ukaguzi wa kabla ya safari ya ndege ya abiria ya Jeju Air saa chache kabla ya kuanguka nchini Korea Kusini, na kuua watu 179, ulimeonyesha kuwa ndege hiyo ilikuwa haina shida yoyote,” shirika hilo la ndege limesema.

“Hakuna shida yoyote iliyobainika kwenye gia ya kutua,” Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Kim Yi-bae aliuambia mkutano wa wanahabari mjini Seoul, huku uchunguzi ukiendelea kujua kwa nini magurudumu hayakushuka ilipotua kwa dharura.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Bangkok wakati ilitua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan siku ya Jumapili, na kuwaka moto na kuua kila mtu aliyekuwemo, isipokuwa wafanyakazi wawili, baada ya kuruka ukuta.

Wachunguzi bado wanafanya kazi ya kubaini kilichosababisha ajali mbaya zaidi ya ndege kuwahi kutokea nchini Korea Kusini.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *