Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amewapongeza Plymouth kwa kuwapa changamoto licha ya kupata ushindi wa 3-1 na kusonga mbele katika Robo Fainali ya kombe la FA
“Pongezi kubwa kwa Plymouth kwa kufanya kazi yetu kuwa ngumu sana,”
“Walikuwa na mpangilio mzuri katika nafasi zao ingawa tumeshinda,” amesema Guardiola.
Plymouth waliwashtua viongozi wa Ligi ya Premia Liverpool katika duru iliyotangulia na walikuwa kwenye ari nzuri huko Etihad pale Maksym Talovierov alipowafunga kwa kichwa dakika ya 38.
Huku City wakiwa na tumaini pekee la kupata ushindi, waliwapa wasiwasi mashabiki wao huku Erling Haaland akiwa miongoni mwa wale walioachwa kwenye benchi.
Hata hivyo, ni mmoja wa vijana wa City Nico O’Reilly alileta matumaini baada ya kufunga magoli mawili na Kelvin De Bruyne akitupia lingine.

