Klabu ya Simba imepata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mechi hiyo imechezwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Shujaa wa mechi alikuwa Steven Mukwala aliyefunga magoli yote ‘ hat trick’ na kuifanya Simba kupunguza pengo la pointi 4 dhidi ya Yanga wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 58.

