Kiungo wa Chelsea, Moises Caicedo, amesema bado ana uwezo wa kuongeza makali zaidi kwenye mchezo wake kwa kufunga mabao na kutoa pasi za mabao, licha ya kutajwa na mashabiki wengi kuwa moja ya viungo bora zaidi wa ulinzi duniani.
Caicedo, mwenye umri wa miaka 24, ameanza kuonyesha thamani ya dau la pauni milioni 115 alilonunuliwa nalo kutoka Brighton mwaka 2023, baada ya kuwa mchezaji muhimu katikati ya uwanja chini ya kocha Enzo Maresca.
Amesema haoni kama yeye ndiye bora duniani, lakini anaamini anaweza kufanya zaidi:
“Nahitaji kuonyesha mambo mengi zaidi. Najua ninaweza kutoa pasi za mabao na kufunga,” alisema.
Caicedo ametumia mfano wa mchezo dhidi ya Tottenham ambapo alipambana kuokoa mpira na kutoa pasi ya goli kwa Joao Pedro.
Kuhusu mjadala wa kumfananisha na kiungo wa Arsenal, Declan Rice, Caicedo amesema hana tatizo na kulinganisha:
“Ni mchezaji mzuri sana. Itakuwa vita nzuri kati yangu na yeye.”
Chelsea wanakabiliana na Arsenal Jumapili, na Caicedo anaamini wanaweza kuwashusha kasi vinara hao:
“Kwa nini isiwezekane? Hatujawakutana bado,” alisema kwa kujiamini.

