Phil Foden aliibeba Manchester City baada ya kutupia mabao mawili muhimu, ikiwemo la dakika za majeruhi, na kuipa timu ushindi wa 3-2 dhidi ya Leeds. City waliongoza 2-0 kipindi cha kwanza kupitia Foden na Josko Gvardiol, lakini Leeds walirejea mchezoni kipindi cha pili na kusawazisha kupitia Calvert-Lewin na Nmecha.
Hata hivyo, Foden alizima matumaini ya Leeds akifunga kwa mkwaju mzuri nje ya eneo la boxi, akihakikisha City wanaondoka na pointi tatu muhimu katika mbio za ubingwa.

