Bi harusi auawa siku moja kabla harusi Ufaransa

Bi harusi auawa siku moja kabla harusi Ufaransa

Bibi harusi aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia harusi yake katika kijiji karibu na mji wa kusini-mashariki wa Ufaransa wa Avignon baada ya watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao kufyatua risasi, maafisa wa eneo hilo walisema.

Mshukiwa mmoja wa shambulizi pia aliuawa katika majibizano ya risasi za moto, na bwana harusi na mtoto wa miaka 13 walijeruhiwa vibaya wakati wa tukio hilo katika kijiji cha Goult.

Msako unaohusisha makumi ya maafisa wa polisi na helikopta unaendelea kuwatafuta washukiwa wasiojulikana ambao walifanikiwa kukimbia.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinaripoti kwamba ghasia hizo zinaweza kuhusishwa na mgogoro wa dawa za kulevya.

Mamlaka imefungua uchunguzi kuhusu mauaji na jaribio la mauaji.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *