22 wauawa kwa bomu kanisani

22 wauawa kwa bomu kanisani

Takriban watu 22 wameuawa na wengine 63 kujeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika kanisa moja mjini Damascus, wizara ya afya ya Syria imesema.

Mwanamume mmoja alifyatua risasi kwa kutumia silaha katika Kanisa la Kiorthodoksi la Ugiriki la Nabii Elias katika kitongoji cha Dweila wakati wa ibada Jumapili jioni kabla ya kulipua vilipuzi, kulingana na wizara ya mambo ya ndani.

Ilisema mshambuliaji huyo alikuwa na uhusiano na kundi la wanajihadi la Islamic State (IS).

Hata hivyo, kundi hilo halikukiri kuhusika na tukio hilo.

Picha na video kutoka ndani ya kanisa zilionyesha madhabahu iliyoharibiwa sana, viti vilivyofunikwa kwa glasi iliyovunjika na damu iliyotapakaa kwenye kuta.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *