Balozi Nchimbi awasili Arusha

Balozi Nchimbi awasili Arusha

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili mkoani Arusha na kupokewa na viongozi wa chama na serikali, wakiongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndugu Dadi Musa Matoroka (kulia pichani) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paul Makonda, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kisongo Arusha.

Wengine pichani ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha mjini, Dkt. Wilfred Soileli na Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha mjini, Timothy Sanga.

Katibu Mkuu Balozi Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Wanawake Arusha 2025, litakalofanyika jijini humo, siku ya Jumanne, tarehe 24 Juni 2025.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *