Utata bado wagubika maziko ya Lungu

Utata bado wagubika maziko ya Lungu

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amemaliza ghafla muda wa maombolezo ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Edgar Lungu katika hali ya mvutano mkali kati ya familia na mamlaka kuhusu mipango ya maziko yake.

Hatua hii inafuatia kuahirishwa kuwasili kwa mwili wa Lungu kutoka Afrika Kusini na familia yake siku ya Jumatano, na kuacha nchi hiyo kutokuwa na uhakika kuhusu lini na wapi kiongozi huyo wa zamani atazikwa.

Katika hotuba yake Alhamisi jioni, Rais Hakainde Hichilema alitangaza kumalizika mara moja kwa kipindi cha maombolezo, akisema nchi hiyo inahitaji “kurejesha maisha ya kawaida”.

“Serikali imefanya kila iwezalo kuwasiliana na familia ya rais wetu wa sita aliyefariki ,” alisema Hichilema.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *