Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Said Yakubu (kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Afrika katika Baraza la Uongozi la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Kanizat Ibrahim ambaye ni raia wa Comoro.
Balozi alimpongeza kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi hiyo na pia kumueleza namna mpira wa miguu wa Tanzania unavyokuwa kwa kasi chini ya uongozi wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia.

