Nchemba asema TZ imejipanga na mabadiliko ya sera ya Marekani

Nchemba asema TZ imejipanga na mabadiliko ya sera ya Marekani

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) amesema kuwa Tanzania imejipanga kukabiliana na mabadiliko ya sera za nje za Marekani kuhusu misaada kwa nchi za Afrika toka utawala mpya wa Rais Donald Trump uingie madarakani.

Amesema Tanzania itatumia rasilimali zake ndani kupitia Bajeti Kuu ya Serikali.

. Dkt. Nchemba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( IMF ) Bw. Adran Ubisse, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Alisema kuwa Serikali imetenga fedha na kuongeza mafungu ya matumizi kupitia Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, kwa ajili ya kugharamia sekta mbalimbali zinazoathiriwa moja kwa moja na uamuzi huo wa Marekani, ikiwemo sekta ya afya.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *