Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha Alphonce Simbu kwa kushinda nafasi ya pili katika mbio za Boston Marathon.
” Pongezi za dhati kwa Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Kimataifa ya Mbio ya Boston (Boston Marathon),”
” Umefanya kazi nzuri,”
“Ushindi wako ni matokeo ya kujituma kwa bidii, maandalizi mazuri, nidhamu yako kuanzia jeshini, kwenye mazoezi hadi kwenye mashindano, ukilibeba kwa heshima ya hali ya juu jina la nchi yetu,”.
“Endelea kuipeperusha vyema bendera ya Taifa letu,” ameandika Rais Samia.
Simba, ambaye ameshinda zaidi ya milioni 200, amemaliza kwa muda wa 02:05:04 na kushinda nafasi ya pili.
Nafasi ya kwanza imechukuliwa na Mkenya John Korir aliyemaliza katika muda wa 02:04:45

