Ancelotti bado hana mwelekeo

Ancelotti bado hana mwelekeo

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, ambaye amekuwa akihusishwa kutimkia Brazil, amesema kuwa lisema ataweka wazi mipango yake ya baadaye Mei 25 baada ya mchezo wao wa mwisho wa La Liga.

Malengo ya Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 65, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake Madrid, zikiwa zimesalia na mechi tano ni kufikia tofauti ya pointi nne za wapinzani wao Barcelona na kutwaa taji la La Liga.

Kufikia hilo kungewezekana kwa kiasi fulani endapo wasingeshindwa na Barcelona kwenye fainali ya Copa del Rey, na kupokonywa taji la Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa na Arsenal katika robo fainali.

“Nina mapenzi makubwa kwa klabu yangu, wachezaji wangu na mashabiki wetu, na pia heshima kubwa,” Ancelotti aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mchuano wa Madrid wa La Liga dhidi ya Celta Vigo Jumapili.

“Kwa hivyo nitazungumza kuhusu mustakabali wangu tarehe 25 (Mei) na sio kabla.”, amesema.

Real Madrid watawakaribisha Real Sociedad Mei 25 katika mechi yao ya mwisho ya La Liga msimu huu — kisha wataondoka kuelekea Marekani kwa ajili ya Kombe la Dunia la Vilabu litakaloanza Juni 14.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *