Villa yajiokotea kwa Fulham

Villa yajiokotea kwa Fulham

Youri Tielemans amefunga bao pekee kwa kichwa Aston Villa ilipoilaza Fulham 1-0 siku ya Jumamosi na kuongeza matumaini yao ya kumaliza katika nafasi tano bora za Ligi ya Premia na kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji aliunganisha kona ya John McGinn dakika ya 12.

Tielemans nusura atengeneze bao la pili kwa Ollie Watkins lakini bahati haikuwa yao.

Villa wamesalia katika nafasi ya saba wakiwa wamesalia na mechi tatu lakini sasa wana pointi 60 sawa na Nottingham Forest na Chelsea, ambazo zote zina mchezo wa ziada wa kucheza.

Kwa upande mwingine, kipigo hicho kimekuwa ni pigo kubwa kwa matumaini ya Fulham inayoshika nafasi ya nane.

Wana pointi 51 kutokana na michezo 35 lakini wanaweza kushuka chini zaidi kulingana na matokeo mengine wikendi hii.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *