Maafisa wa Upelelezi wa Kupambana na Dawa za Kulevya waliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), wamemkamata Mwanamke mwenye umri wa miaka 25 akijaribu kusafirisha Dawa za kulevya kwenda India.
Mwanamke huyo aliyetambuliwa kama Caroline Wanjiku Mwangi alinaswa alipokuwa akijaribu kupanda Ndege kuelekea Goa, India.
Alipokamatwa, wapelelezi walifungua mzigo wake na kupata Kilo 1.3 za Cocaine. Kwa sasa Wanjiku yuko chini ya ulinzi katika kituo cha Polisi cha JKIA, akisubiri kufikishwa Mahakamani.

