Rais wa Ukraine Volodymyr amekutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer siku ya Jumamosi siku moja tu baada ya Rais huyo kuzozana na Rais wa Marekani Donald Trump walipokutana huko Washington, Marekani.
Rais huyo alipata makaribisho mazuri zaidi katika Mtaa wa Downing mjini London baada ya Zelenskyy kuruka na ndege akitokea Marekani kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Ulaya siku ya Jumapili kujadili mpango wa amani wa Ukraine.
Viongozi wa Ulaya walitoa ujumbe wa kumuunga mkono Zelenskyy na Ukraine muda mfupi baada ya mzozo wake na Trump katika ofisi ya Ikulu Marekani Oval, wakionyesha mpasuko mkubwa kati ya washirika wa jadi wa Marekani na Ulaya kuhusu mzozo huo tangu Trump arudi White House.
Katika mzozo wao, Trump alimshutumu Zelensky kwa kukataa mpango wa amani katika vita dhidi ya Urusi.
Zelenskyy pia atamtembelea Mfalme Charles siku ya Jumapili.

