WANAWAKE TEHRAN WAPEWA MAFUNZO YA SILAHA HUKU MVUTANO WA IRAN NA MAREKANI UKIONGEZEKA

WANAWAKE TEHRAN WAPEWA MAFUNZO YA SILAHA HUKU MVUTANO WA IRAN NA MAREKANI UKIONGEZEKA

Mji mkuu wa Iran, Tehran, umeshuhudia kuanzishwa kwa kambi maalum ya mafunzo inayowalenga wanawake katika Uwanja wa Imam Hussein. Mafunzo haya yanajumuisha mbinu za matumizi ya silaha pamoja na utoaji wa huduma ya kwanza. Lengo kuu lililowekwa wazi na viongozi wa nchi hiyo ni kuwajengea wananchi uwezo wa kujilinda na kuwaandaa kisaikolojia na kimwili kuwa tayari kujitolea kwa ajili ya usalama wa taifa lao.

Katika tukio hilo la kwanza la aina yake, makumi ya wanawake walijitokeza na kushiriki kikamilifu wakiwa wamevalia chador, ambalo ni vazi la asili linalofunika mwili mzima na kuacha uso tu. Serikali ya Iran imesisitiza kuwa programu hiyo ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha jamii ili iweze kukabiliana na hali yoyote ya dharura au kitisho kinachoweza kujitokeza dhidi ya mipaka ya nchi yao.

Uamuzi wa kuendesha mafunzo haya unajiri katikati ya vuguvugu kubwa la kisiasa na kijeshi katika Ukanda wa Mashariki ya Kati. Mvutano huo umeathiri pia uchumi wa dunia, ukichochewa na kauli ya Iran ya kutishia kuendelea kuufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz hadi hapo Marekani itakapokubali na kutekeleza masharti iliyowekewa, jambo lililosababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa.

Ingawa serikali inaeleza kuwa kambi hiyo ni hatua ya kawaida ya kuongeza utayari wa raia, waangalizi wengi wa mambo wanaichukulia kama ishara ya wazi ya maandalizi ya vita au kukabiliana na hali mbaya zaidi inayoweza kutokea kutokana na migogoro inayozidi kushika kasi katika kanda hiyo.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *