Walker wa Man City atimkia Burnley

Walker wa Man City atimkia Burnley

Beki wa Uingereza anayekipiga Manchester City Kyle Walker amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu mpya iliyopanda daraja ya Ligi Kuu ya Uingereza Burnley kwa ada inayoripotiwa ya pauni milioni 5 ($6.8 milioni).

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 35, amecheza mechi 410 kwenye Premier League na kushinda taji mara sita akiwa na City, pamoja na Ligi ya Mabingwa.

Alitumia kipindi cha pili cha msimu wa 2024-25 kwa mkopo katika klabu ya Serie A AC Milan, ambao hawakutumia haki yao ya kumnunua.

Mkataba wa Walker katika klabu ya City, ambayo alijiunga nayo 2017, ulipaswa kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2025-26.

” Tunayofuraha kuthibitisha usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Kyle Walker,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Beki huyo mwenye uzoefu ameweka kalamu kwa mkataba wa miaka miwili

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *