Kinda wa Brazil kutua Chelsea

Kinda wa Brazil kutua Chelsea

Kocha wa Palmeiras, Abel Ferreira amesema kuwa anaamini kuwa kijana mjanja Estevao Willian yuko tayari kukwea pipa hadi Ligi ya Premia baada ya kuaga katika klabu hiyo ya Brazil kwa kufunga bao dhidi ya waajiri wa baadaye Chelsea Ijumaa.

Estevao, 18, alifunga bao zuri la kusawazisha katika robo fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu kati ya timu hizo mjini Philadelphia lakini hakuweza kuzuia Chelsea kushinda 2-1 kutokana na bao la kujifunga.

Sasa atakamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu hiyo ya London, hatimaye kuelekea Uingereza zaidi ya mwaka mmoja baada ya Chelsea kukubali kumlipa Palmeiras kitita cha euro milioni 57 ($67.1m), zikiwemo bonasi.

“Sina watoto wa kiume, nina mabinti wawili, hivyo, namuona kijana huyu kama mwanangu,” Ferreira alisema baada ya mechi hiyo kwenye uwanja wa Lincoln Financial Field, akiongeza kuwa alitupiana maneno na kocha wa Chelsea Enzo Maresca kuhusu Estevao.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *