Waandamana kupinga kukamatwa kwa mpinzani Uturuki

Waandamana kupinga kukamatwa kwa mpinzani Uturuki

Maandamano yametokea nchini Uturuki baada ya mamlaka kumkamata meya wa Istanbul, siku chache kabla ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais.

Ekrem Imamoglu, kutoka chama kisicho na dini cha Republican People’s Party (CHP), anaonekana kuwa mmoja wa wapinzani wakubwa wa kisiasa wa Rais Recep Tayyip Erdogan.

Waendesha mashtaka walimshtumu kwa ufisadi na kusaidia kundi la kigaidi, wakimwita “mshukiwa wa kiongozi wa shirika la uhalifu”.

Polisi waliwakamata watu 100 – wakiwemo wanasiasa wengine, waandishi wa habari na wafanyabiashara – kama sehemu ya uchunguzi.

Imamoglu alisema mtandaoni “mapenzi ya watu hayawezi kunyamazishwa”, akiwatetea wanaoandamana kwa ajili yake.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *