China yawanyonga 4 kwa ishu ya madawa ya kulevya

China yawanyonga 4 kwa ishu ya madawa ya kulevya

Raia wanne wa Canada wamenyongwa nchini China kwa mashtaka yanayohusiana na dawa za kulevya mapema mwaka huu, mamlaka ya Canada imethibitisha.

Wote walikuwa na uraia wa nchi mbili na utambulisho wao umefichwa, waziri wa mambo ya nje wa Canada Mélanie Joly alisema.

Msemaji wa ubalozi wa China nchini Canada aliripotiwa kuitaka Ottawa “kuacha kutoa matamshi ya kutowajibika”, kwani wadadisi walihofia kudorora zaidi kwa uhusiano kati ya nchi hizo baada ya miaka mingi ya mzozo.

Wizara ya mambo ya nje ya China ilisema siku ya Alhamisi kwamba ilichukua hatua “kwa mujibu wa sheria”, huku ubalozi ukisema kuna ushahidi “dhabiti na wa kutosha” kwa uhalifu wao.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *