Donald Trump amesherehekea siku ya 100 ya muhula wake wa pili kwa mkutano wa kampeni huko Michigan.
Wakati wa hotuba yake ya dakika 90 rais hiyo wa Marekani alimkejeli Joe Biden, akidai kuwa alishinda uchaguzi wa urais wa 2020 kimakosa na kutetea uamuzi wake wa kuzitoza ushuru nchi mbalimbali duniani.
Akizungumza mbele ya skrini za kielektroniki zinazosomeka “siku 100 za ukuu”, Bw Trump aliwashambulia wanaompinga na kujigamba kuhusu juhudi za serikali yake “kuwafukuza raia wengi”.
“Ni wajibu wangu adhimu kama amiri jeshi mkuu. Nina wajibu wa kuokoa nchi yetu.”, amesema.

