Slot: Tumehuzunika

Slot: Tumehuzunika

Mkufunzi wa Liverpool Arne Slot amesema kuwa kutolewa kwa timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa kumeleta mshituko, lakini amefarijika kwa kupoteza dhidi ya timu bora ya Paris St Germain katika mchezo mkali wa hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa ulioamuliwa kwa njia ya penati.

Katika kile Slot amekiita mchezo bora katika historia ya kandanda ambapo PSG iliishinda Liverpool 4-1 na kutinga robo fainali, Slot amesema timu yake imepambana kiume.

“Ndio, bila shaka ni mshtuko,” Slot alisema.

“Lakini tumetoka kwa kupambana dhidi ya dhidi ya moja ya timu bora zaidi barani Ulaya,” amesema.

“Timu zote zilicheza vizurin na mwishowe PSG walishinda.”

Kipa wa PSG Gianluigi Donnarumma aliokoa mikwaju ya penalti kutoka kwa Darwin Nunez na Curtis Jones na kuipa ushindi timu yake.

Liverpool walikuwa wameshinda mechi ya mkondo wa kwanza wa wiki iliyopita huko Paris 1-0.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *