Enrique: Liverpool pia walistahili kufuzu

Enrique: Liverpool pia walistahili kufuzu

Kocha wa Paris St Germain, Luis Enrique amesema timu yake na Liverpool zilistahili kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, licha ya timu yake kushinda 4-1 katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Mhispania huyo alifurahishwa na jinsi kikosi chake kilivyojizatiti na kutoka sare ya bila kufungana baada ya mechi ya mkondo wa kwanza wiki iliyopita kuwatoa Liverpool wanaoongoza Ligi ya Premia kwa mabao 4-1 katika mikwaju ya penalti kwenye uwanja wa Anfield siku ya Jumanne.

“Timu zote mbili zilistahili kwenda hatua inayofuata, zimecheza vizuri zaidi,”

“Tulijaribu kucheza kwa uwezo wetu, lakini ilikuwa ngumu kwani wapinzani wetu walikuwa na nguvu,”

” Timu zote mbili zilistahili kufuzu na penati mara nyingi hazina mwenyewe,” amesema.

PSG hawajawahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, walifungwa na Bayern Munich katika fainali ya 2020, huku washindi wa 2019, ambapo Liverpool walipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele baada ya kuongoza jedwali katika awamu ya nane ya ligi.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *