Klabu ya Singida Black Stars itacheza fainali ya kombe la CRDB Bank Federation Cup baada ya kuinyuka Simba Sc kwa mabao 3-1 katika mechi ya Nusu Fainali.
Matarajio ya Simba ilikuwa kushinda na kuifuata Yanga kwa ajili ya kuwania ubingwa wa michuano hiyo.
Kwa matokeo haya, Simba imepoteza ndoto za taji la michuano hiyo na sasa matarajio yao ni taji la ligi Kuu linaloshikiliwa na Yanga.
Katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya kombe la CRDB Federation uliochezwa katika dimba la Kwaraa mkoani Manyara, Singida BS walifanikiwa kuongoza kipindi cha kwanza kwa mabao 2-0, mabao ambayo yalifungwa na mshambuliaji wao Jonathan Sowah dakika ya 17 ya mchezo na Emmanuel Keyekeh dakika ya 35.
Keyekeh alipachika bao la tatu kwa mpira wa adhabu.
Goli pekee la Simba Sc limefungwa na Jean Ahoua
Singida BS sasa watakutana na Yanga Sc kwenye mchezo wa fainali.

