Baada ya minong’ono kuwa hawatocheza mechi leo dhidi ya watani wao Yanga baada ya kudaiwa kutotokea katika mkutano wa kupanga mechi, klabu ya Simba imesema kuwa itacheza mechi hiyo leo Benjamin Mkapa.
Simba wamethibitisha kuwa watacheza mchezo huu wa dabi dhidi ya Watani wao wa jadi Yanga SC.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Simba wamepost picha na kusindikiza na ujumbe uliosomeka:
“Tutakuwepo”
Mashabiki wanategemea kwenda kutazama mechi hii majira ya jioni.
Je, unatabiri nini?
