Rais wa Uingereza adai kutekwa Kenya

Rais wa Uingereza adai kutekwa Kenya

Raia wa Uingereza ameiambia BBC kuwa yeye na raia kadhaa wa Uturuki walitekwa nyara katika mji mkuu wa Kenya Nairobi na watu waliojifunika nyuso zao siku ya Ijumaa, huku raia hao wanne wa Uturuki wakiwa bado hawajapatikana.

Necdet Seyitoğlu, ambaye aliishi nchini Uingereza kwa miaka 18 kabla ya kuhamia Kenya miaka miwili iliyopita, alisema aliachiliwa baada ya saa nane alipowaonyesha wanaodaiwa kumteka nyara nakala ya pasipoti yake ya Uingereza.

Katika taarifa iliyotoleqa, Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilisema “wanatoa usaidizi wa kibalozi kwa Muingereza na familia yake kufuatia tukio lililotokea nchini Kenya”.

Polisi wa Kenya waliambia BBC kuwa wanachunguza “tukio la utekaji nyara” baada ya dereva wa pikipiki kushuhudia utekaji nyara huo.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *