Rais Samia kununua m20 kila goli Simba

Rais Samia kununua m20 kila goli Simba

Katika kuongeza hamasa ya ushindi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Rais Samia atatoa milioni 20 kwa kila goli ambalo klabu ya Simba itafunga katika mechi za Nusu Fainali ya kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Stellenbosch kutoka Afrika Kusini.

Akizungumza kuhusu mchezo huo muhimu utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar, Msigwa amesema:

“Kama kawaida, hii ni nusu fainali. ‘Goli la mama’ katika CAFCC ni shilingi milioni 20 kwa kila goli la ushindi. Simba, kazi ni kwenu — shindeni mechi hii twendeni fainali.”

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni. Simba SC itaingia uwanjani kuwakabili Stellenbosch wakiwa na malengo makubwa ya kutinga fainali na kulinda heshima ya Tanzania katika michuano hiyo ya kimataifa.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *