Rais Samia aipa tano Simba kufuzu Fainali

Rais Samia aipa tano Simba kufuzu Fainali

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Simba kwa kufuzu fainali Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufanikiwa kupata sare ya 0-0 dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini na kupata tiketi ya kufuzu fainali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia ameandika;

“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup), na kuandika historia ya kufika fainali ya mashindano haya.

“Mmeipa nchi yetu heshima kubwa,”

“Nawatakia kila kheri. Mnayo hamasa yangu wakati wote.”.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *