Manchester City itamenyana na Crystal Palace katika fainali ya tatu mfululizo ya Kombe la FA baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Nottingham Forest Uwanja wa Wembley.
Kikosi cha Pep Guardiola kilipata bao la kuongoza la mapema kupitia kwa Rico Lewis na bao la Josko Gvardiol la kipindi cha pili likahitimisha mafanikio ya nusu fainali.
City wanaweza kutazamia kumenyana na Palace kwenye Uwanja wa Wembley mnamo Mei 17 baada ya The Eagles kushinda 3-0 dhidi ya Aston Villa katika nusu fainali nyingine Jumamosi.
Fainali yao ya 14 ya Kombe la FA inaipa City nafasi ya kushinda shindano hilo kwa mara ya nane na ya tatu tangu Guardiola alipowasili 2016.

