Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe amechaguliwa tena kuwa Rais wa shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
Motsepe ambaye amekuwa Rais wa shirikisho hilo tangu mwaka 2021, sasa atasalia katika kiti hicho mpaka mwaka 2029 kwa awamu ya pili mfululizo.
Uchaguzi huo umefanyika leo Machi 12,2025 Jijini Cairo nchini Misri katika mkutano mkuu usio wa kawaida wa 14 wa CAF.
Viongozi kadhaa akiwemo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na CECAFA Wallace Karia, Rais wa Yanga SC na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika Mhandisi Hersi Said pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’ wameshiriki uchaguzi huo.

