Mkuu wa Wilaya awachukulia hatua msibani bodaboda wasiovaa kofia

Mkuu wa Wilaya awachukulia hatua msibani bodaboda wasiovaa kofia

Katika hali isiyotegemewa, Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Mh. Mbarack Batenga ( pichani) ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata waendesha pilipiki waliokuwa msibani bila kuwa na kofia ngumu ( helmet).

Akiongea katika msiba huo wakati wa kuaga miili sita ya wanafunzi waliogongwa na basi wakiwa mazoezini, ameliagiza Jeshi la Polisi, kuwachukulia hatua bodaboda wote waliofika kuomboleza ila hawana kofia ngumu wasiruhusiwe kuendesha pikipiki zao bali wasukume mpaka wanapofika nyumbani kwao.

Baada ya maagizo hayo Jeshi la Polisi, lilianza kutekeleza agizo kwa haraka kwa kusimama kwenye njia zote zinazoruhusu waombolezaji kuondoka.

Mh.Batenga ametoa maagizo hayo ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuanza kudhibiti ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva na madereva wenyewe kuvunja sheria za barabarani.

” Somo linaanzia hapa hapa, waliokuja msibani kwa tunawashukuru,”

” Lakini wasiokuwa na kofia hakuna kuendesha, wasukume pikipiki zao mpaka nyumbani na polisi isimamie,'” alisema.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *