Mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini, George Mkuchika ametangaza rasmi kutogombea tena nafasi ya ubunge baada ya kutumikia katika nafasi hiyo kwa miaka 20 .
Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Newala na katika mikutano yake anayoifanya jimboni humo, Mkuchika ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum amesema ameamua kutogombea nafasi hiyo kutokana na umri alionao, lakini yupo tayari kuwa mshauri kwa yeyote atakayetaka ushauri wake.

