Kipa wa Brazil Alisson, ambaye alilazimika kutoka nje ya uwanja baada ya kugongana kwa vichwa wakati wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Colombia Alhamisi katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia, ameiacha timu ya taifa na atarejea katika klabu yake ya Liverpool, timu hiyo ya Ligi ya Premia imesema.
Alisson na mlinzi wa Colombia Davinson Sanchez wote walianguka baada ya kugongana vichwa wakati wa kipindi cha pili.
Wahudumu wa afya walikimbia uwanjani kuwatibu, kabla ya wachezaji wote wawili kubadilishwa.
Ripoti za vyombo vya habari zilisema Alisson, 32, alitolewa kama tahadhari baada ya kuhisi kizunguzungu kufuatia jeraha hilo.
“Alisson anasafiri kurudi Merseyside na atafanyiwa tathmini kutoka kwa wahudumu wa afya wa Reds,” Liverpool ilisema katika taarifa.
Alisson baadaye aliwatoa hofu mashabiki wake al “Hey guys, ni kuwajulisha tu kuwa niko sawa! Lazima tu kufuata itifaki ya vipimo,”
” Asanteni sana kwa kunitakia heri,” alichapisha kwenye page yake ya Instagram.

