Liverpool Yapata Ushindi Bila Kummhitaji Salah

Liverpool Yapata Ushindi Bila Kummhitaji Salah

Liverpool ilipata ushindi muhimu wa 2-0 dhidi ya West Ham huku Mohamed Salah akianzia benchi. Alexander Isak alipunguza presha kubwa juu yake kwa kufunga bao lake la kwanza kwenye EPL tangu ajiunge na klabu, huku Florian Wirtz akionesha ubora mkubwa katikati ya uwanja.

West Ham walianza kwa kujilinda na kutegemea mashambulizi ya kushtukiza, lakini Liverpool walimiliki mpira bila tishio kubwa katika kipindi cha kwanza. Baada ya mapumziko, Wirtz alitoa pasi murua iliyomfungulia Gakpo, na mwishowe Isak kufunga kwa ustadi.

Paqueta kupata kadi nyekundu kulivunja kabisa matumaini ya West Ham, na dakika za lala salama Gakpo akafunga la pili kupitia mpira wa Joe Gomez. Liverpool walimaliza mchezo bila hata kuhitaji nguvu ya Salah, wakikatiza mfululizo mbaya wa matokeo.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *