Arteta Amkabidhi Hincapie Majukumu Mazito

Arteta Amkabidhi Hincapie Majukumu Mazito

Arsenal imepata pigo kubwa baada ya William Saliba kuumia mazoezini na kukosa mchezo muhimu dhidi ya Chelsea. Gabriel pia hayupo, hivyo Arteta analazimika kuanza na Pierro Hincapie pamoja na Christhian Mosquera kwa mara ya kwanza kama beki wa kati kwenye Premier League.

Habari njema kwa Arsenal ni kwamba Gabriel Jesus na Viktor Gyokeres wamerejea kikosini na watakaa benchi. Jesus anarudi baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha la ACL, wakati Gyokeres anatarajiwa kuongeza nguvu katika ushambuliaji baada ya timu kumtegemea Mikel Merino kwa wiki kadhaa.

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *