Klabu ya Yanga imemuajiri kocha wa zamani wa Angola , Pedro Goncalves kuwa mkufunzi wao mpya akichukua nafasi ya Romain Folz.
Mkufunzi huyo wa Ureno amechukua mikoba ya kocha wa muda Patrick Mabedi, ambaye alikuwa akishikilia ngome hiyo kufuatia kutimuliwa Folz, aliyekuwa kocha mkufunzi msaidizi wa Mamelodi Sundowns.
Gwiji huyo wa zamani wa Kaizer Chiefs Mabedi aliongoza Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwashinda Silver Strikers kutoka Malawi 2-0 Jumamosi na kwa jumla ya 2-1 ( aggregate).
Yanga pia imemteua Filipe Pedro kuwa kocha msaidizi.
Habari zinasema Mabedi bado atakuwa kwenye jopo moja la makocha wa timu hiyo.
Kocha huyo wa zamani wa Malawi alijiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara wiki mbili zilizopita.

