Meneja wa Borussia Dortmund, Nuri Sahin amesema kuwa anabeba lawama kwa kipigo cha 5-2 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid siku ya Jumanne, akisema kwamba uamuzi wake wa kuimarisha safu yake ya ulinzi huku akiongoza 2-0 ulikuwa na matokeo katika kupoteza kwao kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo.
Dortmund waliingia kwenye mchezo wa Jumanne wakiwa nyuma ya ushindi mara mbili mfululizo na kuanza msimu wa Ligi ya Mabingwa lakini wakabwagwa na Real Madrid katika mechi ya marudiano ya fainali ya msimu uliopita.
Wenyeji walifunga mabao matano kufuatia uamuzi wa Sahin kuwatoa Donyell Malen na Jamie Bynoe-Gittens na kuwaingiza mlinzi Waldemar Anton na kiungo mkabaji Pascal Gross mapema kipindi cha pili.
“Sio rahisi kuelezea, kwa kweli,”
“Vijana walifanya vizuri, wakafunga mabao mawili na kwenda mapumziko, lakini kipindi cha pili kilikuwa cha fedheha kwetu kwa sababu ya ulinzi dhaifu,”, amesema.

