Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti amemsifu Vinicius Jr baada ya fowadi huyo wa Brazil kufunga hat-trick kipindi cha pili na kuwasaidia kujikwamua kutoka mabao mawili nyuma na kuwalaza wageni Borussia Dortmund 5-2 katika Ligi ya Mabingwa.
Ancelotti aliuambia mkutano na waandishi wa habari kuwa ana uhakika kwamba Vinicius mwenye umri wa miaka 24 angeshinda tuzo ya Ballon d’Or ya mchezaji bora zaidi duniani Jumatatu.
“Ninachoweza kusema ni kwamba ni nadra kuona mchezaji anayecheza kipindi cha pili na kufanya kama Vinicius alivyofanya,”
” Na si kwa sababu ya mabao matatu bali kwa sababu ya ubora wake; ni mchezaji wa ajabu,” Ancelotti alisema.

