Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu imeahirishwa hadi Novemba 3, 2025.
Hatua hii ni baada ya upande wa Jamhuri kusema hawana shahidi wa nne katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

